Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tafiti mpya iliyofanywa na taasisi ya IFOP kwa usaidizi wa Msikiti Mkuu wa Paris, imechunguza aina mbalimbali za ubaguzi dhidi ya Waislamu wanaoishi Ufaransa, na matokeo yake yamekuwa ya kushtua, kwani yanaonyesha kuwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) inazidi kuongezeka nchini humo.
Katika utafiti huo, swali kuu lilikuwa:
“Je, unafikiri kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita umewahi kuwa mwathirika wa vitendo vya kibaguzi?”
Asilimia 66 ya Waislamu wa Ufaransa walijibu ‘ndiyo’, wakati ni asilimia 18 tu ya wafuasi wa dini nyingine waliotoa jibu kama hilo.
Sababu za ubaguzi zilivyotajwa na washiriki:
1- 50% walihusisha ubaguzi huo na dini yao (Uislamu)
2- 25% walihusisha na uraia wao wa sasa au wa kudhaniwa
3- 22% walihusisha na rangi ya ngozi yao
Kuenea kwa chuki dhidi ya Waislamu
Ripoti hiyo imeonesha kuwa ubaguzi dhidi ya Waislamu unaendelea kuongezeka nchini Ufaransa. Waandaaji wa ripoti wametumia neno “Muslimophobia” badala ya “Islamophobia” ili kusisitiza kuwa mashambulizi haya yanalenga mtu binafsi kwa sababu tu ya kuwa Mwislamu au kuonekana kama Mwislamu, bila kujali kiwango chake cha imani au ibada.
Njia ya ukusanyaji wa takwimu
Tafiti hii ilifanywa kupitia:
1- Mahojiano ya simu na Waislamu 1,005
2- Na dodoso la mtandaoni lililojibiwa na takriban Waislamu 1,000 wanaoishi Ufaransa, mwaka 2023.
Imejaza pengo ambalo mashirika ya kupinga ubaguzi yamekuwa yakilalamikia kwa muda mrefu, kwani takwimu rasmi za serikali ya Ufaransa huzingatia tu malalamiko yaliyoripotiwa rasmi, na si uzoefu halisi wa waathirika wengi.
Takwimu kuhusu malalamiko rasmi
Licha ya kiwango kikubwa cha ubaguzi:
1- Ni asilimia 66 tu ya Waislamu walisema wangetoa malalamiko rasmi wakikumbwa na ubaguzi.
2- Kwa wale waliokwisha pata uzoefu wa ubaguzi wa kidini, kiwango cha kuwasilisha malalamiko kinashuka hadi 58%.
Maeneo yenye ubaguzi mkubwa zaidi:
1- Ukaguzi wa utambulisho na polisi kwa misingi ya muonekano
2- Mchakato wa kutafuta ajira
3- Kutafuta makazi
Takwimu rasmi za serikali kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni
1- Julai iliyopita, serikali ya Ufaransa ilitangaza kuwa matukio ya chuki dhidi ya Waislamu yaliyoandikishwa hadi nusu ya mwaka 2025 yameongezeka kwa asilimia 75 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
2- Mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya watu yameongezeka mara tatu.
Katika miezi 5 ya kwanza ya mwaka huu (2025):
1- Matukio 145 ya chuki dhidi ya Waislamu yameripotiwa.
2- Katika kipindi kama hicho mwaka 2024, yalikuwa 83 tu.
3- Mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya watu yameongezeka kwa 209%, kutoka mashambulizi 32 mwaka jana hadi 99 mwaka huu — yakichukua zaidi ya theluthi mbili ya matukio yote ya chuki dhidi ya Waislamu.
Your Comment